HISTORIA YA SHULE
Shule yetu Bright Angels Secondary School iliyochini ya shirika lisilo la kiserikali(NGo) la WHITE ANGELS INVESTMENT
linalomilikiwa na watanzania wajasiliamali na wenye malengo ya kuendeleza elimu katika wilaya yetu ya Mkuranga na Taifa kwa ujumla; ilianzishwa mwaka 2005 kama kituo cha masomo ya ziada, katika eneo la Soweto - Vikindu
(Mkuranga).
Kwa sasa tunapatikana katika kijiji cha Kisemvule - kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga; kilometa moja (1) kutoka
barabara kuu ya Kilwa.
Mahitaji ya elimu yalipelekea kuanzisha sekondari katika mfumo rasmi na kupata usajili wake mwaka 2007 kwa namba S3556. Maendeleo yake yamekuwa ya mafanikio kwa maana vijana wetu wote wanafanikiwa kupata vyeti na wengi kuendelea na masomo kidato cha tano na vyuo mbalimbali hasa kwa upande wa sayansi.
Kutokana na uhitaji mkubwa wa watu kujiendeleza kielimu tulilazimika kusajili pia kituo cha watahiniwa wa kujitegemea na kupata namba ya usajili P2878 kwa program za mtihani wa maarifa (QT), watahiniwa wa kujitegemea kidato cha nne na kidato cha tano na sita kwa mwaka mmoja. Program hii ya watahiniwa wa kujitegemea inaendelea kwa asubuhi na jioni kwa wafanyakazi
Program hizi zimekuwa na manufaa kwa jamii kwani hadi sasa kuna watumishi wengi wa serikali wakiwemo walimu,
wanasheria, waandishi wa habari, nk ambao wamepitia programu hii hapa shuleni na kwenda katika vyuo mbalimbali
hapa nchini kama vile chuo kikuu Dar es salaam(UDSM) na matawi yake ya CHANG’OMBE (DUCE), IRINGA (MUCE)
chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) na matawi yake ya IRINGA (RUCO), TABORA, SONGEA, MTWARA, chuo kikuu Dodoma (UDOM). Na vyuo vingine mbalimbali katika ngazi ya cheti na Diploma.
Taasisi hii ni ya kijamii, malengo yetu ni kusaidia zaidi jamii ya kitanzania kwaajili ya maendeleo ya taifa letu la
Tanzania. Tunawakaribisha wote ili tuijenge nchi yetu kwa kuwaelimisha vijana wetu ili kuwa na wataalamu mbalimbali katika nyanja tofauti kwa maendeleo yetu.
Tunahimiza watoto kuwa na nidhamu nzuri ili kujenga taifa la watu wenye nidhamu na utii kwa watu mmoja mmoja,
jumuiya na taifa kwa ujumla.
